Fuata maagizo yaliyo hapa chini ili usanidi printa yako.
Usanidi wa Maunzi
Angalia mwongozo wa usanidi wa karatasi kwa maelezo kuhusu kusanidi maunzi ya printa, kama vile kujaza wino au kuweka katriji za wino na kupakia karatasi.
Usakinishaji wa Viendeshi
Sakinisha viendeshi wakati umemaliza usanidi wa maunzi ya printa. Viendeshi viko kwenye CD hii katika njia zifuatazo:
Kiendeshi cha Printa
\Driver\Printer\Driver
Kiendeshi cha Kichanganuzi (Printa inayoweza kufanya kazi anuwai pekee)
\Driver\Scanner2\Driver
Fax Utility (Printa inayoweza kufanya kazi anuwai pekee)
\Apps\FaxUtility
PCL au PS3(PostScript3) Kiendeshi cha Printa (Printa inayokubaliwa peke yake):
Baadhi ya vipengele vya uchapishaji havipatikani na viendeshi vya PCL na PS3. Ili utumie vipengele vyote vya uchapishaji, sakinisha kiendeshi cha printa kilichotajwaa hapa juu.
Angalia Mwongozo wa Mtumiaji ili uhakikishe printa yako inakubali PCL au lugha za chapa za PS3, na kisha ufuate maagizo ili usakinishe kiendeshi.
|
Kiendeshi cha Printa cha PCL
\Driver\PCLUniversal\
au
\Driver\Universal\
Kiendeshi cha Printa ya PS3(PostScript3)
\Driver\PostScript
Muunganisho wa Mtandao na Usanidi
Unganisha kebo ya LAN au utumie paneli thibiti ya printa ili uunganishe kwa njia ya pasi waya kwenye mtandao. Pakua na uendeshe EpsonNet Config ili usanidi mipangilio ya mtandao.
Pakua Miongozo na Programu
Unaweza kupakua miongozo na programu zingine kutoka kwenye tovuti za usaidizi wa Epson.